NALAZIMIKA kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kushiriki mafunzo ya siku tano ya Internet na Uhusiano wake na uandishi wa habari wakati huu wa dunia ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ambapo internet ni kila kitu.
Elimu ya Internet ni muhimu sana kwa maisha ya waandishi wa habari kwani kama alivyosema Rupert Murdoch alipokuwa akihutubia wahariri wenzake wa magazeti nchini Marekani; “Utafika wakati hakuna atakayekuwa na haja ya kununua gazeti kwa sababu maendeleo ya sayansi na teknolojia yanamuwezesha kupata habari na taarifa yoyote aitakayo.”
Hii ina maana kuwa mwandishi wa habari asiyefahamu elimu ya Internet ni kama vile anajitia katika mazingira magumu ya kufanya kazi zake. Hii ni elimu muhimu sana kwani kwa Internet, mtu anapata taarifa ya tukio wakati linatokea na hivyo kuepuka kupata taarifa zilizopotoshwa.
Nimenufaika sana na mafunzo haya, ingawa siwezi kusema nimepata kila nilichokitarajia. Siku tano za mazunzo hazikutosha kunijenga vizuri isipokuwa nilichopata ni mwanzo wa safari ndefu ya kujifunza ili nipate kubobea katika matumizi ya Internet kufanikisha kazi zangu. Mkazo zaidi nitauweka katika kufahamu kwa vizuri zaidi namna ya kuandika makala zangu kwa kuunganisha viunganisho (links) vya kihabari kwa ajili ya kuwaongoza wasomaji wangu na wale watakaotembelea blogu yangu mpya niliyoanzisha wakati wa mafunzo haya, kwenye upataji wa taarifa zaidi kwa kile nilichokiandika.
Kwa yote haya, nafurahia kazi nzuri ya mwalimu wetu mkuu katika mafunzo, Peik Johansson wa Shirika la Utangazaji la Finland akifanyia Radio Finland kwa kutujenga taaluma ya Internet na Maggid Mjengwa, Mtanzania anayeishi Iringa na kijana mweledi wa Internet na mwana blogu maarufu nchini Tanzania. Wamenijenga nguvu kubwa.
ON the outset, I must thank God for enabling me to attend the five days Internet workshop being among about 15 editors from various media houses in Tanzania. The workshop, or rather, the training, was very good. It provided me with good opportunity to learn something which I have never thought of placing myself to learn.
Internet knowledge is a very essential component for any modern time journalist to know. As one Rupert Murdoch, American editor, once said to his colleagues, “it will reach a time when nobody would have interest in reading newspaper because of the technological advancement of internet”, for a journalist to lack knowledge of the internet, is like bringing self into uncalled for situation.
Via internet, one gets desired news and information and would not mind to by a newspaper or tuning to radio or television to get the same. Internet enables one to see incidents at the time of occurrence, something very fantastic, in that, no distortion.
The benefit I got from the training is a good start and this pushes me to build keen interest in learning more how to use internet to do journalism effectively and efficiently. I am saying there is need to learn more because 5 days could not give me everything I expected, and by that I should say that I need more time to learn more on the way I link my material with various websites.
This would help to lead my readers and those who would-be visitors of my new blog which I introduced during course of the training, to get more information of what I wrote.
I thank so much our training instructors, Mr. Peik Johansson from Finnish Broadcasting Company YLE Radio Finland who taught us Internet & its relations in journalism, and also Mr. Maggid Mjengwa, a Tanzanian residing in Iringa and a renowned blogger in the country. They provided me with BIG ENERGIZER!
Friday, November 14, 2008
Maoni khs Mafunzo
NDANI ya darasa, wakati mwalimu akifundisha, baadhi ya washiriki walipata nafasi ya kupiga picha maendeleo ya mafunzo. Picha kama hizi zilitumika kusaidia washiriki wa mafunzo kujifunza namna ya kuzituma kwenye blogu zao. Hii ilikuwa ni sehemu muhimu ya mafunzo kwa wahariri waliohudhuria mafunzo ya siku tano ya utendaji kazi ya habari za uchunguzi kwa kutumia Internet.
Haya ni matokeo ya ukuaji wa teknolojia ya mtandao wa kompyuta katika kurahisisha shughuli za utaafutaji, uandaaji na usambazaji wa habari mbalimbali kwa manufaa ya wasomaji wa magazeti na wasikilizaji wa redio na televisheni.
Lazima tukubali kwamba mafunzo aliyotupa mwalimu wetu, Keip Johansson, yalikuwa na manufaa makubwa kwa ajili ya kutujenga kitaaluma. Tushuruku basi waandaaji na wafadhili wa mafunzo haya adhimu. Yalikuwa mafunzo ya maana sana na ambayo yalikuja kwa wakati wake hasa, kwani fani ya uandishi wa habari imejikuta katika mabadiliko makubwa kutokana na mapinduzi ya teknolojia.
Maoni kama haya nilipata kuyasikia hivi karibuni kutoka kwa waandishi waliohudhuria mafunzo ya kwanza kama haya mwezi Agosti mwaka huu kwenye ukumbi tuliokuwepo safari hii, wa Tanzania Global Development Learning Centre (TGDLC) ndani ya majengo ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tanzania (IFM).
Subscribe to:
Posts (Atom)