Wednesday, November 12, 2008

Mafunzo kwa Internet

Kusema kweli tangu Jumatatu nimeingia katika dunia mpya. haya mafunzo ninayopata kupitia Peik JOHANSSON, ni mazuri ajabu. waandishi wa TZ tumekuwa nyuma sana katika mambo haya ya kujikita vilivyo kwa Internet. sasa tunajua makosa tulofanya, lazma tuamke kwenda mbele. Internet ni kila kitu kama alivyosema Rupert MURDOCH katika hotuba yake kwa Jukwaa la Wahariri la Marekani Agosti 2005.
Tukaze kamba katika kuchimba mambo kupitia Internet. najua tukimaliza Ijumaa, tutakuwa wahariri/waandishi wa namna nyingine tofauti na tulivyoingia TGDLCentre hapa IFM. Tunalazima ya kuwapa dole waandaaji na wafadhili wa mafunzo haya adhimu kwelikweli.

No comments: