Friday, November 14, 2008

Maoni khs Mafunzo


NDANI ya darasa, wakati mwalimu akifundisha, baadhi ya washiriki walipata nafasi ya kupiga picha maendeleo ya mafunzo. Picha kama hizi zilitumika kusaidia washiriki wa mafunzo kujifunza namna ya kuzituma kwenye blogu zao. Hii ilikuwa ni sehemu muhimu ya mafunzo kwa wahariri waliohudhuria mafunzo ya siku tano ya utendaji kazi ya habari za uchunguzi kwa kutumia Internet.

Haya ni matokeo ya ukuaji wa teknolojia ya mtandao wa kompyuta katika kurahisisha shughuli za utaafutaji, uandaaji na usambazaji wa habari mbalimbali kwa manufaa ya wasomaji wa magazeti na wasikilizaji wa redio na televisheni.

Lazima tukubali kwamba mafunzo aliyotupa mwalimu wetu, Keip Johansson, yalikuwa na manufaa makubwa kwa ajili ya kutujenga kitaaluma. Tushuruku basi waandaaji na wafadhili wa mafunzo haya adhimu. Yalikuwa mafunzo ya maana sana na ambayo yalikuja kwa wakati wake hasa, kwani fani ya uandishi wa habari imejikuta katika mabadiliko makubwa kutokana na mapinduzi ya teknolojia.

Maoni kama haya nilipata kuyasikia hivi karibuni kutoka kwa waandishi waliohudhuria mafunzo ya kwanza kama haya mwezi Agosti mwaka huu kwenye ukumbi tuliokuwepo safari hii, wa Tanzania Global Development Learning Centre (TGDLC) ndani ya majengo ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tanzania (IFM).

No comments: